January 28, 2017


MPIRA UMEKWISHAAA


-Manula anafanya maajabu anaokoa mpira uliokuwa unajaa wavuni, konaa...Inachongwa tena, hakuna kitu
-Kipa Manula yuko chini pale akitibiwa

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 90, Simba wanafanya shambulizi hapa, Mavugo anatwanga kichwa lakini Manula anaokoa na kuwa kona hapa, sasa  Azam FC wako nyuma wote
Dk 88, Simba wanapoteza nafasi nzuri kabisa, mpira wa adhabu wa Kichuya, Mavugo yeye na lango anapaisha hapa

Dk 85, Azam FC wanaonekana kuzidi kuimaisha ulinzi kwa kuwa wachezaji sita sasa wanabaki nyuma kufanya ulinzi
SUB Dk 83, Abdallah Kheri, kinda matata huyu anaingia kuchukua nafasi ya Bocco ambaye ameshindwa kurejea baada ya kuumia
KADI Dk 82 Mwamuzi Onoka wa Arusha anamlamba kadi ya njano Aishi Manula kwa kupoteza muda
Dk 80, Bocco yuko chini hapa akiwa ameshika paja lake
Dk 78, Zimbwe anapokea pasi na Mavugo, anawatambuka mabeki wa Azam na kuachia mkwaju lakini hakulenga lango
SUB Dk 76, Simba wanamuingiza Mudathir kuchukua nafasi ya Kingue ambaye ameumia


Dk 73, Stephan KIngue wa Azam yuko chini anatibiwa hapa, anatolewa nje na huenda asirejeeGOOOOOOOOOOO Dk 70, Bocco anamtambuka Mwanjale na kuachia mkwaju mkali wa chinichini na kuandika bao kwa Azam FC
Dk 68, Simba wanafanya shambulizi tena, krosi nzuri, Ajib yeye na lango anashindwa kupiga kichwa kulenga. GAoal kick
Dk 68, Yahaha anaingoia vizuri hapa lakini hata spidi hapa, mpira unawahiwa na Agyei
Dk 67, Simba wanafanya shambulizi kali hapa lakini shuti la Kichuya linatoka na kuwa goal kick
Dk 66, Kichuya anageuka na kuachia mkwaju hapa lakini Manula anaudaka vizuri hapa


SUB Dk 65, Simba wanamtoa Liuzio na nafasi yake inachukuliwa na Mavugo
SUB Dk 62, Yahaya Mohammed anaingia kwa upande wa Azam FC kuchukua nafasi ya Singano
Dk 60, Ajibu anapata pasi nyingine nzuri, lakini mwenyewe anaupoteza tena mpira huo
SUB Dk 59, Simba wanamtoa Boukungu na nafasi yake inachukuliwa na Ibrahim Ajibu ambaye mpira wa kwanza tu, anapoteza hapa
 DK 58, Zimbwe wa Simba yuko chini hapa anatibiwa na Himid Mao ambaye tayari ana kadi ya njano


Dk 54, mechi imesimama kwa dakika moja baada ya Bocco kumtwanga teke Boukungu wakati akiachia shuti kwa lengo la kufunga. Inaonekana ilikuwa ni bahati mbaya
Dk 51, mpira unaonekana kuchangamka sasa, timu zinaanza kufunguka na kucheza mipira mirefu na kufanya mashambulizi
Dk 48, Simba wanafanya shambulizi kali, Liuzio anaachia mkwaju mkali hapa, Manula anauficha
SUB Dk 46, Simba inafanya mabadiliko ya kwanza, Shiza Kichuya anaingia kuchukua nafasi ya Jamal Simba Mnyate 

MAPUMZIKODAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45, Bokungu anapiga krosi maridadi hapa ya outer lakini Aishi anadaka vizuri kabisa
Dk 44, Manula anafanya kazi nzuri kwa kutokea na kuudaka mpira wa krosi kabla haujamfikia Athanas
KADI Dk 43, Singano naye analambwa kadi ya njano kwa kucheza faulo dhidi ya Banda

Dk 41, Athanas anamgeuza Yakubu ndani ya boksi, anaachia mkwaju unagonga mwamba kwa juu na kuwa goal kick
Dk 39, Simba wanaingia eneo la hatari la Azam, Muzamiru anaachia shuti lakini linakuwa nyanya hapa kwa Manula
Dk 36 sasa, bado si mechi ya kuvutia sana kama ambavyo ilikuwa imetarajiwa


KADI Dk 33, Erasto Nyoni analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Pastory Athanas, hii ni kadi ya kwanza ya njano ya mchezo huu
Dk 30, hakuna timu iliyogusa nyavu na mpira unaendelea kuchezwa katikati zaidi ya uwanja na tahadhari kubwa yenye uoga ikiendelea kuchukua nafasi
Dk 23, Yakubu anautoa mpira nje na kuwa kona ya kwanza ya mchezo ambao wanaipata Simba. Inachongwa hapa Azam FC wanaokoa


DK 20 sasa, kila timu iko makini sana. Maana walinzi ni wanne kwa kila upande na kila timu inaposhambuliwa inakuwa na walinzi zaidi ya watano
Dk 15, Mahundi anapoteza nafasi nzuri ya kwanza baada ya kuupata mpira kwenye boksi la Simba mabeki wakiwa wamezubaa, anapiga shuti la chini, mpira unampita Agyei na kuwa goal kick
Dk 13, Bocco anajaribu hapa katika lango la Simba lakini Agyei anakuwa makini na kuudaka mpira huo


Dk 9, Bukungu anaachia shuti kali lakini linatoka nje. Kinachoonekana timu hizi kila mmoja imejaza watu wengi zaidi nyuma, hivyo kufanya kusiwe na ladha ya juu ya ushambulizi
Dk 6 sasa, hakuna shambulizi hata moja kali. Zimbwe wa Simba anatolewa nje baada ya kugongana na Mhundi, anapatiwa matibabu
Dk 2, Azam FC wanakuwa wa kwanza kufika lango la Simba lakini shuti la Mahundi, linadakwa kwa ulaini na kipa Agyei
Dk 1, mechi imeanza taratibu kabisa huku kila timu ikionekana inataka kuusoma mpira au mbinu za mwenzake kabla ya kuzipambanua zake


HEAD TO HEAD SIMBA VS AZAM FC
Kutana mara 17
Simba shinda mara 8
Azam Mara 4
Sare 5

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic