January 23, 2017Bilionea kijana zaidi barani Afrika, Mtanzania Mohammed Dewji ameshinda tuzo ya Kiongozi Bora Afrika katika hafla iliyofanyika jijini Zurich nchini Uswiss.

Dewji maarufu kama Mo ameshinda tuzohiyo inayojulikana kwa jina la African Leadership Person of The Year ambayo hutolewa kwa wafanyabiashara au viongozi wanaofanya vizuri.

Mo ameshinda tuzo hiyo ambayo ni heshima kubwa kwake kwa kuwa watu kadhaa maarufu walikuwa wakipewa nafasi ya kuitwaa.

Mfanyabiashara huyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MeTL Ltd, hivi karibuni aliweka dau la Sh bilioni 20 kutaka kununua hisa asilimia 51 katika klabu ya Simba.

Kabla amekuwa mdhamini na mfadhiri wa klabu hiyo akiwa msaada mkubwa wakati ikifika hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuing’oa Zamalek.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV