January 23, 2017Beki wa Simba, Abdi Banda, amesema licha ya kupishana pointi mbili na wapinzani wao Yanga, wachezaji wote wa timu hiyo wanaamini ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu unakwenda Msimbazi.

Simba inaongoza msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 45 huku watani wao Yanga wakiwa na pointi 43, wakiwa wamepishana pointi mbili kati ya nane walizokuwa wamepishana awali.

Banda amesema hawahofii kupishana pointi mbili na Yanga na badala yake wanahitaji kukaza buti kwa kujituma ili waweze kufanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu.

“Kila mechi kwetu ni fainali kuhakikisha hatutoi nafasi kirahisi ya kufungwa kwani tunahitaji kuona tunafanikiwa kuibuka mabingwa msimu huu, kwa kuwa kila mchezaji anapenda kuona tunafanikiwa kutimiza malengo yetu.

“Pointi mbili tulizopishana na Yanga haziwezi kutuzuia sisi kuweza kuibuka na ubingwa kwani wao wanapigana na sisi tunapigana pia.


“Malengo ni kuisaidia Simba kuweza kuchukua ubingwa msimu huu ambapo hata kwa upande wangu nitakuwa na kitu cha kujivunia hapo baadaye katika maisha yangu ya soka,” alisema Banda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV