January 2, 2017


Haras El Hodood ya Misri imetupia mtandaoni na kueleza kuwa mshambuliaji Ibrahim Ajibu ni mchezaji wao mpya.

Ajibu anaonekana akiwa kwenye picha na wachezaji wengine wa Haras El Hodood ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Misri.

Hata hivyo, Msemaji wa Simba, Haji Manara amelifafanua jambo hilo kwa kusema Ajibu bado ni mali ya Simba.

“Nimeliona hilo suala, naulizwa sana. Lakini ukweli Ajibu bado ni mali ya Simba, bado hatujakaa mezani na hao ndugu zetu kuhusiana naye,” alifafanua.

Simba ilitoa ruhusa ya Ajibu kwenda kufanya majaribio hadi Desemba 31, 2016 na baada ya hapo kama amefuzu, pande hizo mbili zingekaa mezani.


Lakini tayar Haras El Hodood ilitangaza kwamba Ajibu alifuzu vipimo vya afya. Hivyo lilibaki suala la benchi la ufundi kuamua.

1 COMMENTS:

  1. page ya haras el hodood ndio ina like 9 tu. msiwafanye mshabiki wa soka wazembe kiasi hicho.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV