January 2, 2017Kiungo mwenye kasi wa Simba, Shiza Kichuya ameweka bayana kuwa kutofunga bao katika mechi tatu mfululizo ambazo ni sawa na dakika 270 kunasababishwa na ushindani uliopo kwa wapinzani wao ambao wengi wao wanacheza kwa tahadhari na kujilinda sana lakini anafurahia kuona wenzake wanafunga huku yeye akihusika kwenye mabao hayo.

Kichuya ndiye kinara kwenye chati ya ufungaji akiwa sawa na washambuliaji wa Yanga, Simon Msuva na Amissi Tambwe ambapo kwa pamoja wana mabao tisa waliyoyafunga kwenye mechi 18 za ligi mpaka sasa.

Winga huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amesema kuwa, hali ya ‘ubutu’ iliyomkuta imechangiwa na mabadiliko makubwa ya timu kwenye kipindi hiki cha mzunguko wa mwisho ambapo kila mmoja anajitahidi kucheza kwa umakini kwa ajili ya kuhakikisha hawafungwi.

“Siyo kama sifungi kwa sababu kiwango kimeshuka, hapana ila tu sasa hali ya ushindani imebadilika kwa sababu kila timu inakomaa kuona haifungwi na hata kama ikipoteza basi siyo kwa mabao mengi, jambo hilo ndiyo limechangia mpaka sasa kwenye mechi tatu sijafunga bao lolote.

“Lakini hata hivyo bado nina furaha kwa sababu timu inapata ushindi na wenzangu wanafunga na tunaendeleza kupata pointi tatu ambazo ndiyo lengo letu kwenye kila mechi na suala la kufunga siyo muhimu sana japo itakapotokea nafasi nitafanya hivyo,” alisema Kichuya.    


1 COMMENTS:

  1. maneno kuntu sana kuonesha ameanza kukomaa kisoka, kila heri Kichuya sote tunaona jinsi unavyoipigania SIMBA kwa moyo wa dhati kabisa na mimi kama mwanachama wa SSC nakuombea DUA sana

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV