January 15, 2017

MKURUGENZI MTENDAJI WA MULTICHOICE TANZANIA, MAHARAGE CHANDE AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI MWANDAMIZI WA CHAMPIONI, WILBERT MOLANDI.


Kampuni ya Multichoice Tanzania inayouza Ving’amuzi vya DSTV, imevishukuru vyombo vyote vya habari vya hapa nchini kwa ushirikiano wao kwa muda wote wa mwaka 2016 uliomalizika hivi karibuni.

Shukurani hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande katika hafla fupi iliyofanyika jana Jumamosi kwenye Ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Chande alisema: “Sherehe hii ambayo awali tulitaka tuifanye kabla ya mwaka 2016 kwisha, ni maalumu kwa ajili ya kuwashukuru wanahabari wote pamoja na vyombo vya habari vya hapa nchini tulioshirikiana kwa mwaka mzima, kusema ukweli mmetubeba tena sana.“Nakumbuka tangu Juni 15, mwaka jana wakati natambulishwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, vyombo vyote vya habari viliandika vizuri kwa kunikaribisha, na kuanzia hapo mpaka leo tumekuwa pamoja, matumaini yetu ni kwamba, mwaka huu utakuwa mzuri kwetu sote na kufanya mambo makubwa zaidi ya mwaka uliopita.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV