January 16, 2017
Straika nyota wa Yanga, Amissi Tambwe, amebakiza miezi minne amalize mkataba wake wa kuitumikia klabu hiyo ambayo alijiunga nayo msimu wa 2014/15 akitokea Simba.

Hata hivyo, Tambwe kabla ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga wa kuongeza mkataba mwingine wa kuendelea kuitumikia timu hiyo, hivi karibuni amepokea ofa kwenda kujiunga na timu moja inayoshiriki ligi kuu ya nchini Algeria.

Tambwe amesema kuwa ofa hiyo ameipata kupitia kwa wakala wake lakini ameshindwa kufanya maamuzi mpaka hapo atakapoiona ofa atakayopewa na klabu yake ya sasa ya Yanga ambayo pia ilimuahidi kumpatia dau zuri baada ya kumalizika kwa mkataba wake.

“Bado sijafanya mazungumzo yoyote yale na uongozi kuhusiana na mkataba mpya lakini kuhusu kufanya mazungumzo na timu za nje hilo ni kweli, kuna timu moja inanitaka hata viongozi wa Yanga wanalijua hilo.

“Viongozi wa timu hiyo kutoka Algeria waliwahi kuja siku chache baada ya dirisha dogo la usajili kufungwa na walipowaambia viongozi wangu wanisajili lakini nitajiunga nao baada ya kumalizika kwa msimu huu wa ligi kuu  walikataa, hivyo kwa sasa wamekuja tena ila bado sijawakubalia mpaka nitakapopata ofa ya Yanga,” alisema Tambwe huku akikataa kuitaja timu hiyo.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV