Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, leo anatarajiwa kupandishwa tena kizimbani kwa mara ya pili ndani ya wiki moja na siku kadhaa, lakini safari hii ikiwa ni kuhusiana na makosa ya Idara ya Uhamiaji.
Manji ni mfanyabiashara maarufu nchini ambaye yuko katika msukosuko mkubwa ndani ya hizi wiki mbili. Wiki iliyopita, Manji alipandishwa kizimbani kwa kesi ya kudaiwa kutumia madawa ya kulenya.
Habari za uhakika zimeeleza Manji ambaye inaelezwa
atapandishwa baada ya kukaa chini ya ulinzi mkali wa maofisa wa polisi na wale wa uhamiaji.
Akiwa katika wodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Muhimbili, Manji alikuwa akilindwa na askari wawili wa Uhamiaji na wanne na wa kaiwada, mmoja tu akiwa anaonekana na mavazi ya kiaskari.
Lakini jana askari waliongezeka na kufikia wanane na kufanya eneo hilo kuwa na ulinzi mkali.
Askari walikuwa ndani ya chumba chake, angalau wawili. Kwenye korido walikuwa wanakaa wawili na wengi wawili hadi watatu walikuwa chini wakiendelea kuzunguka eneo hilo wakiwa na mavazi ya kawaida.
Hali hiyo wakati fulani ililalamikiwa na madaktari wa taasisi hiyo kwamba inawakwaza wagonjwa wengine.
0 COMMENTS:
Post a Comment