- Michuano ya Kombe la FA imetinga hatua ya robo fainali au raundi ya 6 na sasa vigogo Manchester United watakutana na Chelsea katika hatua hiyo.
Man United ambao wamewang’oa Blackburn kwa kuwachapa mabao 2-1, wanakutana na Chelsea katika mechi zitakazopigwa kati ya Machi 10 hadi 13.
Arsenal wanaonekana kupata mchekea kwa kuwa wakiishinda Sutton wanakutana na Lincoln City huku Tottenham walioishindilia Fulham kwa mabao 3-0 yote yakifungwa na Harry Kane, wakiwa wamepangiwa kucheza na Millwall.
- RATIBA
- Chelsea v Manchester United
- Middlesbrough v Huddersfield or Man City
- Tottenham v Millwall
- Sutton or Arsenal v Lincoln City
0 COMMENTS:
Post a Comment