February 23, 2017Kimekaa Kikao cha Bodi ya Kusimamia na Kuendesha Ligi, kiliketi mwanzoni mwa wiki hii na kufanya tathmini ya mambo mbalimbali yaliyotokea kwenye michezo mbalimbali ya mpira wa miguu kwa michuano yote – Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.

Kuna ambao wamekumbana na rungu la adhabu kama ifuatavyo.

Mechi namba 49 (Polisi Mara vs Singida United FC). Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Enock Mwanyonga, na Mwamuzi Msaidizi Namba Mbili, Abdulaziz Ally wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Daraja la Kwanza baada ya kushindwa kumudu mchezo huo.


Uamuzi huo umefanywa kwa mujibu wa Kanuni ya 38(1a) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.


Mechi namba 56 (Singida United vs Alliance Schools FC). Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Omari Miyala, na Mwamuzi Msaidizi Namba Mbili, Innocent Mwalutanile wamefungiwa miaka miwili kwa kushindwa kumudu mchezo huo. Uamuzi dhidi yao umezingatia Kanuni ya 38(1a) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.


Naye Kamishna Hamisi Kambi ameondolewa kwenye orodha ya Makamishna wa Ligi Daraja la Kwanza kwa kushindwa kutoa taarifa ya mchezo huo kwa usahihi. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 39(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Kamishna/Mtathmini Waamuzi.Klabu ya Alliance Schools FC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kugoma kuinbia kwenye chumba vya kubadilishia (changing room), hivyo kusababisha timu yako ikaguliwe kwenye gari. Adhabu imezingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Daraja la Kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV