Young Africans Sports Club kupitia katibu mkuu wake Boniface Charles Mkwasa, inawaomba radhi wanachama wote, wapenzi na mashabiki wa klabu yetu pendwa Young Africans kwa matokeo ya Jumamosi dhidi ya Simba SC kwa kupoteza 2-1.
Klabu inawaomba kuwa watulivu na pia inashukuru sana kwa utulivu mliouonyesha na kutii sheria zote kwenye mchezo wa Jumamosi.
Matokeo haya tuliopata ni ya kimchezo kikubwa ni kupambana na michezo iliyobaki mbele yetu na kuendelea kuwapa sapoti vijana wetu kwani bado tuna mashindano mengi na michezo mingi mbeleni.
Tunaamini Mwalimu ameona mapungufu kwenye mchezo uliopita na atayafanyia kazi kuelekea michezo ijayo na tutafanya vizuri na kurejesha furaha yetu.
Uongozi unaamini wanachama na wapenzi wa Yanga wataendeleza utulivu na kuendelea kuipa sapoti timu yao kama ilivyo jadi yao.
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano.
Young African Sports Club.
0 COMMENTS:
Post a Comment