Shabiki wa Simba, mfanyakazi wa Hoteli ya Protea alianguka na kupoteza maisha baada ya Shiza Kichuya kufunga bao la pili dhidi ya Yanga.
Simba ilitoka nyuma kwa bao moja, ikafunga mawili kupitia Laudit Mavugo na Kichuya na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Suleiman Victor alikuwa akisikiliza mpira kupitia redio ya EFM, alianguka na kupoteza maisha wakati akishangilia.
Wafanyakazi wenzake walijitahi kumuwahisha katika Hospitali ya Tumaini enero la Upanga, lakini tayari alipoteza maisha.
Msemaji wa TFF, Alfred Lucan naye alithibitisha hilo.
“Ni kweli tumepata taarifa za shabiki huyo, ni taarifa za masikitiko. Tumeelezwa baada ya kuanguka wakati anashangilia, aliuathiri ubongo wake,” alisema.
Bao la Kichuya lilifungwa katika dakika ya 81 baada ya kutokea pembeni mwa uwanja na kuachia mkwaju mkali.
0 COMMENTS:
Post a Comment