February 13, 2017



Baada ya kupita miaka 17, hatimaye Singida United imefaniwa kurejea Ligi Kuu Bara msimu ujao ambapo kocha mkuu wa timu hiyo, Fred Felix Minziro amezichimba mkwara mzito timu zinashiriki ligi hiyo zikiwemo Simba, Yanga na Azam kuwa zijipange kweli kwani Singida United hii si ya mchezomchezo.

Singida ambayo imekata tiketi ya kucheza ligi kuu kwa kufikisha pointi 30 katika Kundi C ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye kundi hilo, juzi Jumamosi iliifunga Alliance mabao 2-0 ambapo mchezo wa mwisho itapambana dhidi ya Mvuvumwa.

Minziro aliyewahi kuwa mchezaji na kocha wa Yanga, amesema kuwa anashukuru Mungu kufanikiwa kuipandisha timu hiyo huku akizitaka Simba, Yanga na Azam kujipanga vizuri kwani wanatambua shughuli yake.

“Kiukweli  tunashukuru Mungu kwa kuweza kuwafunga wapinzani wetu na kurejea ligi kuu baada ya miaka 17 kupita, naamini hii itakuwa zawadi kwa watu wa Singida kuweza kuziona Simba, Yanga na Azam zikicheza mkoani mwao.


 “Lakini kwa upande wangu imekuwa faraja kubwa kurejea tena ligi kuu baada ya misimu mitatu kupita kutokana na kufundisha Panone kabla ya Singida na hakuna asiyejua uwezo wangu ila kwa kuwa nimerejea tena wapinzani wangu wajipange vizuri kwani sitataka kufanya mzaha wowote,” alisema Minziro.

SOURCE: CHAMPIONI 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic