February 21, 2017





Na Saleh Ally
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys imefanikiwa kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Mataifa Afrika itakayofanyika nchini Gabon.

Michuano hiyo imepangwa kufanyika Mei, mwaka huu.
Mara kadhaa nimetoa pongezi baada ya Serengeti Boys kufuzu. Ni jambo la kujivunia na mwanga mkuu kwa Tanzania.

Lakini ninachokiona ni kwamba Tanzania imefuzu kucheza michuano hiyo wakati haina stamina ya kutosha katika suala la maendeleo ya vijana.

Kwamba mafanikio yameonekana juu, lakini chini hakuna maandalizi ya kutosha kuwandeleza vijana ambao watafanya vizuri baada ya hao wanaoendelea kufanya vema.

Hakuna akademi bora za vijana, hakuna viwanja vizuri vya vijana wetu kuchezea na hakuna michuano bora iliyoandaliwa.

Achana na ile michuano iliyoanzishwa na Shirikisho la Soka Tanzania kwa kuwa viongozi wake waliona ni wakati mzuri wa kampeni na wanataka kujisafisha.

Ilionyesha wazi hakukuwa na maandalizi ya kutosha, ndiyo maana uliona hadi walioumia uwanjani wanabebwa na gari la zimamoto.

Lakini kama watoto watakaokwenda kushiriki michuano ya Gabon, watakaporejea wataungana na nani, watakwenda kucheza wapi? Na yapi mazingira sahihi kwa ajili yao.

Hii inaonyesha bado hakuna mwendelezo ulio sahihi. Hofu yangu watoto hao pamoja na juhudi zao wasije wakatumika kama sehemu ya kampeni za TFF iliyofeli kurejea madarakani.

Kama wakirudi nchini, wakasajiliwa na klabu kubwa. Je, kuna mazingira sahihi ya kuwaendeleza?

Ninawakumbusha hili kwa kuwa vijana wengi wamepotea na walikuwa na vipaji vizuri kabisa. Kama unakumbuka michuano ya Copa Coca Cola na wengine walikwenda hadi wakatwaa ubingwa.

Kumbuka wengi waliokwenda kwenye michuano ya Afrika Kusini. Nao walipotea hivihivi. Hivyo kuna namna ya kufanya ili kuweka mambo yawe sahihi.

Baada ya vijana hao kurejea nchini. Basi kuwe na mazingira ya mwendelezo huku kukiwa na mazingira sahihi ya uzalishaji na uendelezaji wa wengine.

Hapa ninazigusa klabu pia, si TFF pekee. Lazima tujue hakuna mwendelezo wa vijana ambao unaishia kwenye michuano tu.

Viongozi wa klabu, nanyi mnapaswa kuwa na timu bora za vijana zenye mwendelezo badala ya mambo ya kubahatisha tu huku mkisubiri wanaopikwa ili muwachukue na baada ya muda muwatelekeze.

gumzia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic