February 21, 2017


Kipa Wayne Shaw ametimuliwa na klabu ya Sutton United.

Sutton United imetolewa kwenye michuano ya Kombe la FA baada ya kufungwa kwa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal na Shaw alikuwa katika bench akila pizza au pie.

Shaw alionekana akila msosi wakati mechi inaendelea na imeelezwa kwamba alifanya hivyo kwa kuwa alibeti.

Kitendo hicho kinaonekana kuwa ni magumashi na hatari kwa mchezo wa soka.


Uchunguzi wa awali unaonyesha Shaw alibeti kupitia Sun Bets na sasa tayari Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya England, imeanza uchunguzi kupitia kampuni hiyo ya betting.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic