February 26, 2017Beki juuko Murshid ametua nchini na kujiunga na kikosi cha Simba.

Juuko anaongeza nguvu katika kikosi hicho baada ya kukaa nje kwa muda mrefu.


Beki huyo Mganda alikwenda Gabon kushiriki michuano ya Afcon akiwa na The Cranes, lakini tokea hapo aliendelea kubaki Uganda.

Kabla ya mechi dhidi ya Yanga, Simba walikuwa wakihaha kumpata mtu wa kuziba pengo la Method Mwanjale ambaye ni majeruhi.

Hata hivyo, inaelezwa ilikuwa vigumu kumrejesha Juuko kwa hofu ya kuua morali ya timu. Nafasi yake akapewa Novaty Lufunga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV