February 22, 2017

KAMANDA MPINGA AKIWA NA MHARIRI MTENDAJI WA GLOBAL PUBLISHERS, SALEH ALLY AMBAYE PIA NI BALOZI WA RSA. MABALOZI WA KUJITOLEA WA USALAMA BARABARANI.

Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi, Mohammed Mpinga, amefunguka kuwa, michuano ya soka aliyoianzisha ya Mpinga Cup imeweza kuwanufaisha wengi kutokana na jinsi inavyoendeshwa.

Michuano hiyo ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka, imekuwa ikizishirikisha timu za waendesha bodaboda kutoka maeneo mbalimbali.


Akizungumza na Global TV Online juzi Jumatatu, Kamanda Mpinga alisema: “Lengo la mashindano haya lilikuwa ni kutoa elimu ya usalama barabarani hasa wale vijana wanaoendesha bodaboda, hivyo tunashukuru kumekuwa na mabadiliko makubwa.

“Tunapoendesha michuano hii, pia tunatoa elimu ya usalama barabarani, hivyo wale wahusika wanapata fursa ya kupata mambo mawili kwa wakati mmoja."



Kamanda Mpinga ambaye amekuwa akifanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika jeshi hilo upande wa usalama barabarani, pia alipata nafasi ya kushuhudia uandaaji wa magazeti ya Global Publishers.

Pia alieleza namna ambavyo amekuwa akivutiwa na kulifuatilia kila linapotoka gazeti namba moja la michezo nchini la Championi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic