February 22, 2017
Kampuni ya simu za mkononi inatarajia kumwaga mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuidhamini klabu ya Yanga.


Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza, Mwenyekiti wao, Yusuf Manji tayari aliwaeleza baadhi ya watendaji wake nia ya namna ambavyo Yanga inaweza kufaidika na udhamini mkubwa wa zaidi ya Sh bilioni 4.


“Mwenyekiti alikuwa na mpango huo, alishazungumzia suala hilo hapo awali. Lakini kumekuwa na mambo kadhaa yaliyotakiwa kumalizia.


“Hata sisi mwanzo hatukujua ni Tigo kwa kuwa hakuwa ameeleza kama ni kampuni gani ya simu. Lakini baadaye tuligundua ni Tigo,” alieleza mmoja wa viongozi ndani ya Yanga.


“Lengo lake ni Yanga kuwa kubwa Afrika na bila udhamini ni sawa na kujidanganya. Hivyo kama mmiliki wa Tigo, ni rahisi Yanga kupata udhamini huo ingawa ninaamini kama kampuni ingedhamini hata timu nyingine.


“Kwa sasa, labda tusubiri misukosuko ipungue ndiyo mwenyewe anaweza kuzungumza. Maana sasa yuko Hospitali, mara mahakamani hivyo hajatulia.”


Manji kwa sasa analezwa kuwa mmiliki halali wa Tigo baada ya kuinunua katika mnada mwaka 2014 mwishoni.Lakini kuna kesi imefunguliwa ya kuanzisha upya mnada wa ununuzi wa kampuni hiyo ukidaiwa kuwa una walakini.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV