February 17, 2017



Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ndiye aliyemkomboa Mwenyekiti wao, Yusuf Manji kwa kumuwekea dhamana yenye thamani ya Sh milioni 10, jana.

Manji alifikishwa mahakamani jana akituhumiwa kutumia madawa ya kulevya.

Mkwasa ambaye ni mchezaji na kocha wa zamani ndiye aliyefanya juhudi hizo akishirikiana na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na maofisa wengine wa Yanga.

Manji aliingia Mahakama ya Kisutu akiwa kwenye gari aina ya Toyota huku magari mengine kadhaa yakifuatia.

Baada ya kesi, aliondoka kutoka enero la viwanja vya mahakama akiwa ndani ya gari aina ya Hammer.








0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic