February 17, 2017







Waandaaji wa Tamasha la Majimaji Selebuka ambalo hufanyika kila mwaka mjini Songea, wametangaza zawadi kwa washindi wa mbio za marathoni kilomita 42 ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na Sh milioni 1.5.


Tamasha hilo ambalo mwaka huu litafanyika kwa mara ya tatu tangu kuanza kwake mwaka 2015, litajumuisha riadha kwa mbio ndefu na fupi, mbio za baiskeli, midahalo katika shule za sekondari, mashindano ya ngoma za asili, maonyesho ya biashara, utalii wa ndani, Majimaji Selebuka Mtu Kwao Forum na Majimaji Selebuka Mkabesa Platform.


Mwandaaji mkuu wa tamasha hilo, Reinafrida Rwezaura (pichani), ameliambia gazeti hili kuwa, mbali na mshindi wa kwanza kuondoka na kitita hicho, mshindi wa pili atakabidhiwa Sh 1,000,000 na wa tatu Sh 500,000.


"Msimu wetu wa tatu tunatarajia kuuanza Julai 23 mpaka 30, mwaka huu ambapo tutatoa zawadi nono kwa washindi mbalimbali wa riadha, mbio za baiskeli, ngoma za asili, maonesho ya ujasiriamali, utalii wa ndani na wengine," alisema Rwezaura.



Katika hatua nyingine, leo Ijumaa washindi watatu wa mbio za baiskeli waliopatikana msimu uliopita ambao ni Salum Miraji, Allen Nyanginywa na Ipyana Mbogela, wanatarajia kwenda nchini Afrika Kusini kushiriki mashindano ya Dis-Chem Ride for Sight 2017.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic