Kauli ya kocha wa Simba, Joseph Omog kwamba walitakiwa kutumia akili ya ziada ili kushinda kwa kuwa hawakwenda kushindwa dhidi ya Yanga hata kama walikuwa pungufu imeonekana kuwafurahisha mashabiki wengi wa Simba.
Kupitia maoni yao waliyotuma kuhusiana na namna Simba ilivyocheza, mashabiki wengi wa Simba wamesema alikuwa shujaa.
Omog ndiye alifanya mabadiliko kadhaa na kuifanya Simba iibuke na ushindi wa mabao 2-1 licha ya pungufu kwa mchezaji mmoja na nyuma ya bao moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment