February 22, 2017

Kesi  ya Miss Tanzania mwaka 2006 na msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu imesogezwa mbele mpaka Machi 15, mwaka huu kufuatia upelelezi wa shitaka lake kutokamilika.

Wema alilifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Februari 9, mwaka huu na kusomea mashitaka matatu ya kutumia madawa ya kulevya ikiwemo kukutwa na msokoto wa bangi kabla  ya kurejea tena leo Jumatano ambapo kesi hiyo imesogezwa tena mpaka Machi 15, mwaka huu.

Kesi hiyo namba 49 iliyosomwa leo mbele ya hakimu, Thomas Simba ambapo upande wa mashtaka  uliowakilishiwa na  Pamela Shinyambala na Costantine Kalula wameomba isogezwe mbele kwa kuwa upelelezi bado haujakamilika ombi lililokuwa kubwa na upande wa mawakili wa mshatakiwa uliokuwa ukiongozwa na Albert Msando akisaidiwa na Mbunge wa Singida, Tundu Lissu.

Hakimu, Simba alisema kuwa mshitakiwa ataendelea kuwa nje kwa dhamana iliopo mpaka hapo kesi itakapotajwa tena.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV