February 21, 2017




Kikosi cha Simba kimeendelea kujifua asubuhi na jioni ikiwa ni maandalizi ya mechi yao dhidi ya Yanga, Jumamosi.


Simba walio kambini mjini Zanzibar, wamefanya mazoezi asubuhi na jioni yakiwa mazoezi ya kujituma hasa.


“Mazoezi yetu ni mazuri na tunaendelea vizuri,” alisema mmoja wa viongozi wa Simba aliyesema yeye si msemaji.


“Mazoezi ni asubuhi na jioni, hii ni programu ya kocha na wachezaji wote wanaendelea vizuri."



Wachezaji wa Simba wanaonekana wako katika hali nzuri na tayari kwa ajili ya mechi ya Yanga ambayo inaonekana tayari kuwavutia mashabiki wengi kwa kuwa tiketi zimekuwa zikinunuliwa kwa kasi kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic