February 21, 2017




Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amewasili katika ofisi za uhamiaji jijini Dar es Salaam ambako amekuwa akifanyiwa mahojiano.

Wakati jana baadhi ya wadau wa soka na waandishi wa habari walijitokeza mahakamani wakiamini atapelekwa kama ilivyojulikana, lakini haikuwa hivyo baada ya kuugua ghafla na kulazimika kutibiwa.

Kutokana na kushindwa kwenda mahakamani, taarifa zilielezwa angepanda kizimbani leo, lakini haikuwa hivyo baada ya kupelekwa Idara ya Uhamiaji ambako ilielezwa alikuwa akihojiwa.

Watu waliokuwa mahakamani, kwa mara nyingine walilazimika kuondoka katika eneo la mahakama baada ya kuona muda wa kazi umeisha.

Taarifa zilieleza bado alikuwa Uhamiaji: “Alichukuliwa Hospitali pale Muhimbili kupelekwa Uhamiaji. Hadi sasa yupo huko.”


Chanzo hicho kilieleza, Manji aliendelea kubaki katika ofifi za uhamiaji, hali inayomfanya kutorejea kwake tokea Alhamisi iliyopita aliporipoti katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam, maarufu kama Sentro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic