Mmoja wa wachezaji ambaye Watanzania watamkumbuka ni Godfrey Bonny ’N.
Kiungo wa zamani wa Prisons ya Mbeya na Yanga ya Dar es Salaam ambaye alichipukia na kuichezea Tukuyu Stars ya Mbeya pia.
Ndanje amefariki dunia na kuzikwa wiki iliyopita lakini moja ya sifa yake, “Hakuwa mtu wa mchezo kazini”.
Nurdin Bakari naye alicheza Yanga, alicheza na Bonny na kamwe hawezi kumsahau alipomrukia teke tumboni.
Ndanje hakuwa amekusudia, alikuwa akiruka kupiga kichwa mpira lakini mbele yake alikuwepo Nurdin akajikuta akimkanyaga tumboni.
Kiungo huyo aliyekuwa mkimya, alikuwa makini muda wote na kamwe hakupenda kubaki na mpira mguuni na badala yake alitumia muda mwingi kupiga pasi za karibu au mbali.
Alionekana ni kama mtu asiye na nguvu sana lakini alikuwa kinga'ng'anizi katika ukabaji.
Achana na kwamba Yanga au TFF walimsahau, lakini ameacha nembo ya uchapakazi kwa vijana wengine ambao walibahatika kumuona au kumsikia.
Mwenyezi Mungu Amrehemu huko alipotangulia.
0 COMMENTS:
Post a Comment