Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji anatarajiwa kupandishwa mahakamani leo kwa tuhuma za kuonekana kuwa anatumia madawa ya kulevya.
Lakini rafiki yake wa karibu amesema kuwa amekuwa akilalamika kuonewa kwa makusudi na kukandamizwa.
“Amekuwa analalamika kwamba anaonewa na inajulikana kuwa ana matatizo ya mgogo na moyo na amekuwa anatumia dawa ambazo zinaweza kuonyesha kuna vimelea.
“Hata hivyo anaonekana ni mtulivu na kwenye leo anafikishwa mahakamani,” alisema.
Blog hii ilimshuhudia Manji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa anarejeshwa hospitali baada ya kuzidiwa tena aliporejeshwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam alikokuwa akishikiliwa tokea Alhamisi iliyopita.
Manji anapanda kizimbani leo ikiwa ni siku mbili baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa moyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment