Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali amesema ni wakati mzuri wa kikosi cha Simba kuhakikisha inafanya vizuri zaidi na kubeba ubingwa.
Dalali ambaye sasa ni maarufu kama Trump amesema kwa kuwa Simba imerejea kileleni, inachotakiwa ni kuhakikisha haipotezi mchezo na itajihakikishia kubaki tena kileleni.
“Tulifikia pengo la pointi nane, tumepoteza hilo jambo ambalo ni baya. Lakini si wakati wa kujilaumu sasa, badala yake ni kupambana na kushinda kila mechi.
“Simba ikishinda kila mechi ni uhakika itarejea kileleni moja kwa moja na kubeba ubingwa,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment