Pamoja na kwamba kocha wa muda wa Leicester City, Craig Shakespeare ameanza vizuri kwa kuitwanga Liverpool kwa mabao 3-1, lakini mashabiki wameendelea kumkumbuka shujaa wao Claudio Ranieri.
Ranieria aliyekuwa kocha wa Leicester na kuipa ubingwa msimu uliopita, alitimuliwa wiki iliyopita baada ya timu hiyo kuyumba na kuanza kuingia kwenye wimbi la kuteremka daraja.
Mashabiki wa Leicester waliingia uwanjani wakiwa wamevaa picha zake, lakini sehemu mbalimbali mitaani, picha zake zilikuwa zimezagaa kuonyesha wanamkubali na kumshukuru pia.
0 COMMENTS:
Post a Comment