February 28, 2017


MASAU BWIRE, MSEMAJI WA RUVU SHOOTING

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano ambako mabingwa watetezi wa taji hilo, Young Africans itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Mbali ya mchezo huo mmoja kwa siku ya Jumatano, ligi hiyo ambayo ni michuano mikubwa nchini, itaendelea mwishoni mwa wiki hii ambako kwa siku ya Jumamosi Machi 4, mwaka huu Simba itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Ukiacha mchezo huo, michezo mingine ya Jumamosi Machi 4, mwaka huu itakuwa ni kati ya Toto Africans na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza huku Kagera Sugar ikiikaribisha Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.


Azam FC pia itacheza Jumamosi Machi 4, mwaka huu na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Chamazi. Mchezo huo utaanza saa 1.00 jioni wakati mechi nyingine zitaanza saa 10.00 jioni.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limerejesha tena mechi za Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Jumapili Machi 5, mwaka huu Mtibwa Sugar itaialika Young Africans kwenye uwanja huo katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.



Mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom utachezwa Uwanja wa Uhuru ambako African Lyon itaialika Mwadui ya Shinyanga wakati Ndanda FC itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic