February 18, 2017



Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, ameisifia kombinesheni ya Abdi Banda na Novalty Lufunga katika beki ya kati ambapo wamepanga kuiboresha zaidi ili wazoeane zaidi kabla ya mechi ya watani wao wa jadi Yanga.


Hiyo, ni baada ya beki wao tegemeo Mzimbabwe, Method Mwanjale kupata majeraha ya enka kwenye mechi dhidi ya Prisons na kuwa kwenye wasiwasi wa kukosa mechi hiyo ya watani.


Mwanjale hakucheza juzi Alhamisi mechi ya Kombe la FA dhidi ya African Lyon ambayo Simba ilishinda bao 1-0.
Katika mchezo huo, Banda na Lufunga walicheza pamoja katika safu ya ulinzi ya kati ya Simba na kufanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Laudit Mavugo.


Akizungumza  Mayanja amesema wamepanga kuiboresha safu hiyo ya ulinzi baada ya kubaini upungufu mdogo katika mechi dhidi ya Lyon ili Banda na Lufunga wawe fiti dhidi ya Yanga.


Mayanja alisema, kama kombinesheni hiyo ikielewana vizuri, basi ana matarajio makubwa ya safu yao ya ulinzi ya kucheza mechi nyingi bila ya kuruhusu mabao.

“Kwanza nianze kwa kusema kuwa, katika timu yetu kuna wigo mpana wa wachezaji na kila mmoja akipata nafasi ya kucheza basi anacheza kwa kuonyesha ushindani uwanjani.


“Kama ulivyoona mechi ya FA na Lyon alikosekana Mwanjale kutokana na majeraha ya enka, lakini tukampanga Lufunga na kucheza vizuri kwa kuelewana na Banda, tumepanga kuendeleza kuiboresha kombinesheni yao ili kuhakikisha wanaendelea kucheza kwa kuelewana,” alisema Mayanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic