February 18, 2017




Hapo kabla straika Laudit Mavugo alikuwa hafungi mabao kwa timu yake ya Simba kiasi cha kuzua shaka kwa mashabiki na makocha, kuona hivyo benchi la ufundi limembadilishia majukumu na sasa anacheka na nyavu anavyotaka.


Ishu ipo hivi, Simba miaka miwili iliyopita ilivutiwa na ufungaji wa Mavugo akiwa na kikosi cha Vital’O ya Burundi na kumzengea kwa muda mrefu bila mafanikio ikitaka kumsajili.


Kama zali kabla ya kuanza kwa msimu huu, dili la Mavugo likatiki na straika huyo akajiunga na Simba, hata hivyo mambo yakawa ndivyo sivyo kwani mchezaji huyo hakuweza kuendelea na kasi yake ya ufungaji.


Sasa Mavugo ana mabao sita katika Ligi Kuu Bara na kasi yake ya ufungaji inaonekana kuimarika kwani amefunga mabao matatu katika mechi tatu za mwisho za Simba.



Alifunga bao moja dhidi ya Majimaji katika ushindi wa mabao 3-0 kwenye ligi kuu, pia aliifunga Prisons bao moja wakati Simba ikishinda mabao 3-0, pia katika ligi na juzi aliifungia timu yake bao pekee dhidi ya African Lyon na kuipeleka Simba katika robo fainali ya Kombe la FA.


Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amesema kuwa, siri ya Mavugo kubadilika na kufunga mabao hayo ni kumbadilishia majukumu na sasa anacheza katikati, siyo pembeni.


 “Mavugo alikuwa hafungi awali lakini kwa sasa amefanikiwa kufunga  kutokana na kumbadilishia majukumu, awali alikuwa akicheza pembeni na sasa tumemuweka kati ili aweze kufunga na kweli anafunga.


“Pia tumekuwa tukimuelekeza nini cha kufanya ili aweze kurekebisha kiwango chake ambacho tumekuwa tukimtaka akibadilishe ili aweze kuwa bora zaidi na ndiyo maana amebadilika,” alisema Mayanja.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic