February 21, 2017Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma ameendelea kujifua ili ikiwezekana aivae Simba.

Yanga itashuka dimbani pale Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi kuwavaa watani wao wa jadi Simba katika mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Ngoma raia wa Zimbabwe anaonekana kupania kupata nafasi ya kurejea uwanjani kuivaa Simba.


Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, ameiambia SALEHJEMBE kwamba Ngoma anapambana.


“Ngoma anajiandaa vizuri sana, ni suala la kuangalia na afya yake iko vipi. Daktari ndiye atasema mwishoni inakuwaje.


“Lakini yeye anafanya mazoezi maalum kuhakikisha anakuwa viti. Siku chache kabla daktari ataeleza inakuwaje.


“Ingawa watu wamekuwa wana hofu, kwamba Ngoma anazuga lakini ukweli Ngoma ni majeruhi na ndiyo maana anaendelea na mazoezi hayo ili arejee,” alisema mjumbe huyo aliyekataa kutajwa jina.Ngoma ni tegemeo la ushambulizi katika safu ya ushambuliajizi na Yanga inaonekana wanahaha vilivyo kuhakikisha anacheza mechi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV