February 22, 2017



Emmanuel Frimpong raia wa Ghana amejiunga AFC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Sweden.

Frimpong anaungana na Mtanzania mwingine, Thomas Ulimwengu anayekipiga katika timu hiyo lakini anajaza nafasi aliyokuwa amewekewa Said Ndemla wa Simba.

Blog ya SALEHJEMBE ilikuwa ya kwanza kuandika AFC ilikuwa ikimtaka Ndemla lakini ilikuwa ikitaka kumchukua na baadaye akiuzwa, basi yenyewe na Simba wagawane.

Lakini hilo, lilionekana kutokubaliwa na viongozi wa Simba na sasa Frimpong anachukua nafasi yake baada ya kujiunga na AFC akitokea Arsenal Tula inayoshiriki Ligi Kuu ya Russia.

Kabla ya hapo, Frimpong alikuwa kiungo wa Arsenal ya England ambayo ilimpeleka kwa mkopo Wolveshampton, baadaye Charlton Athletic  na Fulham.

Mwaka 2014 alijiunga Barnsley na baada ya hapo akaenda Ufa kabla ya kutulia Arsenal Tula akiwa na kiungo au beki wa zamani wa TP Mazembe, Stopilla Sunzu.

Tayari Frimpong ametambulishwa huku mmiliki wa AFC akishuhudia.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic