March 8, 2017


Arsenal wamezidi kuonyesha udhaifu na kushindilia machungu kwenye mioyo ya mashabiki wao baada ya kukubali kipigo kingine cha mabao 5-1 na kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Arsenal wameondolewa na Bayern Munich ambayo iliitwanga Arsenal kwa idadi hiyo ya 5-1 mjini Munich. Leo imerudia ikiwa ugenini London.

Sasa kikosi cha Arsenal chini ya Arsene Wenger kimeng'olewa kwa jumla ya mabao 10-2.

Arsenal walitangulia kufunga kupitia Theo Walcott lakini Bayern walisawazisha kwa mkwaju wa penalti wa Robert Lewandowski, baadaye Arjen Robben, Douglas Costa na Arturo Vidal akashindilia msumari mara mbili.

Arsenal starting XI: Ospina, Monreal, Koscielny, Mustafi, Bellerin, Ramsey (Coquelin), Xhaka, Oxlade-Chamberlain, Giroud (Ozil), Sanchez (Perez), Walcott

Bayern Munich starting XI: Neuer, Rafinha, Javi Martinez, Hummels, Alaba, Vidal, Alonso, Robben (Costa), Thiago (Kimmich), Ribery (Sanches), Lewandowski














0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic