March 7, 2017


Kiluvya United walisema mengi, kwamba leo wataiangushia dhahama Yanga katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

Lakini hadi mechi hiyo inaisha, wamejikuta “wamechungulia” mabao 6-1.

Maneno ya baadhi ya viongozi wake, yalionyesha wamejiandaa na wangeionyesha kazi Yanga.

Lakini Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi alisema leo hawatafanya mzaha.

Obrey Chirwa akatumia nne na Geofrey Mwashiuya na Juma Mahadhi wakapiga moja moja na mwisho ikawa 6-1. Hakuna tena kelele kutoka kwa Kiluvya.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV