March 9, 2017


Pierre-Emerick Aubameyang ni matata sana, maana leo amepiga hat trick na kuiwezesha Borussia Dortmund kuinyoosha Benfica ya Ureno kwa mabao 4-0.

Ushindi huo, jumla unakuwa 4-1 na Dortmund inasonga mbele hadi robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Aubameyang raia wa Gabon alifunga bao la kwanza, la tatu na nne huku la pili likitupiwa na Christian Pulisic.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV