March 28, 2017

MKUDE (KULIA) AKIWA NA KICHUYA.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema uongozi na wachezaji Ibrahim Ajibu na Jonas Mkude, tayari umefikia makubaliano.

Hans Poppe amesema wao na wachezaji hao wawili wamfikia makubaliano, kinachosubiriwa ni suala la mkataba.

“Sasa ni suala la mkataba tu, fedha walizohitaji kupewa tulikubali baada ya mjadala.

“Linalosubiriwa ni suala la kusaini tu. Sasa nikisikia sijui wanakwenda Yanga au vingine nakuwa sielewi. Ndiyo maana nasema basi waende,” alisema Hans Poppe.

Kumekuwa na taarifa, Ajibu alitaka suala la mkataba liwekwe kando katika kipindi hiki hadi hapo baadaye.


Lakini Hans Poppe amesisitiza, wanaamini makubaliano yaliyofikiwa yalikuwa ni mwafaka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV