March 28, 2017


Kwa masikitiko makubwa, beki kisiki wa zamani wa Manchester United,  Rio Ferdinand ameamua kufunguka na kueleza kuhusiana na lifo cha mkewe.

Rio amesema aliumia sana kutokana na kifo cha mkewe, Rebecca na kuseka hakuwa amejiandaa.
Rebecca alifariki dunia Mei, 2015 baada ya kuanza kupambana na ugonjwa wa kansa ya ziwa kwa kipindi kifupi tu. 
Mauti yalimkuta Rebecca ambaye alimuacha Rio na kazi ya kulea watoto wao watatu na Rio amesema hakuwa amejiandaa kwa kuwa hakujua masuala ya malezi ya watoto.

Rebecca alifariki akiwa na umri wa miaka 34 na kuwaacha watoto wake watatu wenye umti wa miaka 10, miaka nane na wa mwisho mwenye miaka mitano.
“Nilipata matatizo mengi sana kwa kuwa siku nimejiandaa, sikutegemea kama hali hiyo ingetokea katika kipindi kile.

“Sikujua mambo ya kubembeleza watoto kama ilivyotakiwa, lakini sikuwa na namna,” alisema Rio mwenye umri wa miaka 38.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV