March 16, 2017Nchi zilizovusha timu 8 katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni nne tu.

Hispania ndiyo imetawala zaidi kwa kuvusha timu tatu, ikifuatiwa na Ujerumani yenye mbili wakati Italia, Ufaransa na Italia zimevusha moja kila moja.

Real Madrid ya Hispania ndiyo mabingwa watetezi na wanaongoza kulitwaa mara nyingi zaidi.

Unaweza kuona kwa mwendo ulivyo, ubingwa huo kuondoka Hispania inaonekana ni kazi ngumu. Lakini kama utaondoka yaani timu zote tatu zikakosa basi nafasi ya pili ni kwa Ujerumani na tatu ni Italia.

Lakini mchezo wa soka una maajabu yake, hauwezi kujua itakuwaje. Tusubiri, lakini kama unaweza, chagua unayoona inaweza kubeba ubingwa mapemaa.

HISPANIA:
Real Madrid, Barcelona, Atletico Madrid

UJERUMANI
Bayern Munich, Borussia Dortmund

ENGLAND:
Leicester

UFARANSA:
Monaco

ITALIA:

Juventus

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV