March 16, 2017Kikosi cha Simba kilicho mjini Arusha, kitafanya mazoezi mara mbili kwa siku ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho dhidi ya Madini FC.


Simba itaivaa Madini FC ya Arusha katika mechi ya Kombe la Shirikisho itakayochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Jumapili.


Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema hawataidharau Madini kwa kuwa hayo ni mashindano na wanajiandaa kwa umakini mkubwa.


“Mazoezi yatakuwa mara mbili kwa siku, hii ni sehemu ya maandalizi. Hii inategemea na programu yetu, wakati mwingine mara moja kwa siku,” alisema.Simba inatarajia kuendelea na ziara za mikoani mara tu baada ya mechi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV