March 30, 2017


Kiungo nyota wa Arsenal ambaye amekuwa akisumbuliwa na nyama za paja, anaweza akawa fiti kuivaa Man City.


Rafiki wa karibu wa Ozil, ameliambia Metro kuwa Ozil amekuwa akifanya kila linalowezekana ili arejee uwanjani wakivaa Man City wikiendi hii.


“Anaumia sana kuona amekaa nje, lakini hana namna kwa kuwa ni maumivu.


“Anafanya sana juhudi ili arejee na kuivaa Man City. Anaamini atasaidia kufanya vizuri.”


Iwapo Arsenal itapoteza dhidi ya Man City, itazidi kuporomoka kutoka nje ya Top Four na kumuingiza Arsene Wenger kwenye dimbwi la kutimuliwa.Ingawa hajasema, lakini inaonekana Ozil amelenga kupambana na kumuokoa Wenger ambaye alimsajili kutoka Real Madrid na kuweka rekodi mpya ya usajili kwa Arsenal.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV