March 29, 2017


Pambano kati ya Anthony Joshua dhidi ya mkongwe Wladmir Klitschko, litakuwa ndiyo kubwa zaidi katika historia ya mchezo wa ngumi nchini England.

Wakali hao watawania mkada wa uzito wa juu wa IBF na WBA (Super), pia IBO na umebaki mwezi mmoja kamili.


Mashabiki 90,000 wanatarajia kujitokeza na kujaza siti zote kwenye Uwanja wa Stadium jijini London. 

Kila upande umekuwa ukiendelea na maandalizi makali huku Klitschko akiwa anajiandaa kuhamia kwenye kambo yake ya Austria.


Joshua naye na timu yake wamekuwa katika maandalizi makali ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV