March 29, 2017Hatimaye Uwanja wa Ndege wa Madeira imezinduliwa upya ukiwa na nina la mwanasoka Cristiano Ronaldo.

Ronaldo aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi, ameshukuru lakini akawaambia waliokuwa wakilaumu, “hakuomba”.

Madeira ni moja ya visiwa vinavyomilikiwa na Ureno na ndipo alipozaliwa Ronaldo.


Awali, baada ya kutangazwa uwanja huo ungepewa jina lake, wako waliokuwa wakipinga.

Mpenzi wa Ronaldo aitwaye, Georgina Rodriguez aliambatana na mama yake mzazi Ronaldo kumuunga mkono.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV