March 4, 2017
Na Saleh Ally
WIKI ya 27 ya Ligi Kuu England imeanza leo Jumamosi lakini gumzo zaidi ya wiki hii ni pale Liverpool watakapokuwa nyumbani Anfield kuwakaribisha katika mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa.


Wakati ligi inakwenda ukingoni, mambo yanabadilika kwa timu zilizo juu kwenye msimamo kwani Arsenal na Liverpool ambao awali walionekana wana nafasi ya kubeba ubingwa, sasa wana hofu ya kubaki katika Top Four.


Kawaida ili uwe bingwa, ni lazima uwe na uhakika wa kuwa Top Four ambayo ni fursa ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, nafasi ambayo kila timu ingependa kuipata.

Arsenal iko katika nafasi ya 4 ikiwa na pointi 50 na ina mechi 25 pungufu moja kwa Liverpool iliyo katika nafasi ya tano ikiwa na pointi 49. Atakayefungwa nafasi ya kuondoka kwenye Top Four inaanzia hapo. Kama Liverpool watapoteza, basi watakuwa wamejichimbia shimo na hofu ya kurejea ndani ya Top Four huenda ikawa kubwa zaidi.


Kama Arsenal watapoteza, basi watakuwa wameshushwa lakini wana mechi moja mkononi inayoweza kuwarudisha kama watashinda. Sare inaweza ikawa ahueni kwa kila mmoja ingawa ushindi ni muhimu zaidi.

Hesabu zinaonyesha timu hizo zina nafasi ya fifty-fifty yaani asilimia 50 kila moja kushinda ingawa hakuna ambayo imekuwa na mwendo mzuri hivi karibuni.


Katika mechi sita zilizopita, Arsenal ambao watakuwa wageni kesho wameshinda tatu, sare moja na kupoteza mbili, hawako vizuri sana. Liverpool nao wameshinda moja tu, sare mbili na kupoteza ni tatu. Hawa unaweza kusema wako “majalala”, hali si nzuri na kunaweza kuwa na swali. Je, wanaweza kuibuka tena leo?Liverpool:
Katika mechi zake 26 ilizocheza, Liverpool imeshinda 14, sare 7 na imepoteza 5 kama ilivyo kwa Arsenal.

Ikiwa nyumbani, Liverpool imeshinda mechi 8, sare 3 na kufungwa moja tu, hii inaonyesha kuna ugumu kuifunga Anfield na Arsenal watalazimika kuweka gia ya mlima.


Ugenini wameshinda 6, sare 4 na kupoteza 4, lakini hii kwao si ishu sana kwa kuwa wako nyumbani.

Hadi sasa, Liverpool ina ubora wa 67% kufunga ikiwa nyumbani na ina nafasi kubwa pia ya kufungwa kwa kuwa ubora wa kumaliza mechi bila ya kufungwa ikiwa Anfield ni 33% pekee.


Inapokuwa nyumbani inaonyesha Liverpool kwa kila mechi ina uhakika wa kupata ushindi kwa 55% na kama unakumbuka ilishinda pia kwa mabao 4-3 ikiwa ugenini dhidi ya Arsenal ingawa kipindi hicho ilikuwa katika kiwango kizuri ukilinganisha na sasa.


Arsenal:
Kikosi cha Wenger kimeshinda mechi 15 za Premier League, kati ya hizo tano ni za ugenini na tisa za nyumbani. Sare mbili nyumbani na imepoteza mbili Emirates.

Jumla ya mechi ilizocheza ni 25 ikiwa imeshinda 15, sare 5 na imepoteza 5 na nafasi ya 32% kubeba ubingwa. Kwa kifupi, asilimia za kubeba ubingwa zimeporomoka kabisa.


Sare tatu zimepatikana ugenini na imepoteza ugenini mara tatu pia. Hivyo uwezekano wa kupoteza kwao upo ingawa si wa juu sana kama ilivyo kwa sare lakini wanaonekana wana uwezo wa kushinda ugenini.

Arsenal inaonekana kuwa na rekodi nzuri ya mechi zake za uganini. Kwani ina uhakika wa 75% wa kufunga mabao ugenini na imefeli kwa 8% kupata mabao ugenini.


Nafasi ya kukusanya pointi ugenini kwa Arsenal ni 58% ikiwa imefunga mabao ya ugenini kwa 52%, hivyo kuifanya timu isiyokuwa na hofu hata kidogo inapokuwa ugenini.


MECHI 6 ZILIZOPITA ZA ARSENAL
Bournemouth 3-3 Arsenal
Swansea    0-4 Arsenal
Arsenal       2-1 Burnley
Arsenal       1-2 Watford
Chelsea      3-1 Arsenal
Arsenal       2-0 Hull City


MECHI 6 ZILIZOPITA ZA LIVERPOOL
Man United 1-1 Liverpool
Liverpool   2-3 Swansea
Liverpool   1-1 Chelsea
Hull City     2-0 Liverpool
Liverpool   2-0 Tottenham

Leicester    3-1 Liverpool

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV