March 21, 2017

 

 Kikosi cha Liverpool kimetua Tenerife na kuweka kambi ya muda kujiandaa na michezo iliyobaki ya Ligi Kuu England.

Tenerife ni moja ya visiwa vilivyo chini ya Hispania na ndiko Mtanzania Farid Mussa anakipiga katika kikosi cha Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania cha Derpotivo Tenerife.


Farid yuko njiani akija nchini kujiunga na Taifa Stars na Liverpool wameanza maandalizi yao kisiwani humo.

Tenerife ni moja ya sehemu za kuvutia duniani, mara nyingi inatawaliwa na joto la mvuke na ina moja ya fukwe za kuvutia.

Kwa kufanya mazoezi Tenerife, Liverpool watapata nafasi ya kujiimarisha lakini pia kupumzika kutokana na ubora wa mwonekano wa kisiwa hicho cha Hispania.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV