March 21, 2017



Baada ya wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki katika michuano ya kimataifa kudondokea katika michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Zanaco FC ya Zambia. Sasa wanakutana na Mouloudia Club d'Alger ya Algeria.

Hii kwa kipindi kirefu hasa katika soka la Afrika si timu maarufu sana lakini imewahi kufanya mengi makubwa.

Ilivyo ni kama timu iliyoamua kurejesha heshima yake na ina nguvu kubwa ya mashabiki na inataka kurejea na kuonyesha nguvu yake barani Afrika.

Mouloudia Club d'Alger inayojulikana kama MC Alger au MCA kwa ufupi ndiyo timu yenye mafanikio zaidi nchini Algeria.

MCA ilianzisha mwaka 1921 ikijulikana kama Mouloudia ChaĆ bia d'Alger, na baadaye tokea mwaka 1977 ikaanza kujulikana kama Mouloudia PĆ©troliers d'Alger na ilipofikia mwaka 1986 ikabadilishwa tena jina na kuanza kujulikana kama  Mouloudia Club d'Alger in 1986. 

Inatumia Uwanja wa Omar Hamadi na ndiyo klabu ya kwanza ya Algeria kushindwa kombe la michuano ya kimataifa baada ya kubeba ubingwa wa Klabu Bingwa ambayo sasa ndiyo Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hii ni moja ya klabu yenye mafanikio zaidi nchini humo licha ya kwamba kuna klabu nyingine kubwa na maarufu kama JS Kabylie, USM Alger na ES Setif.

MCA inatumia rangi nyekundu na kijani, imeshinda makombe saba nchini humo upande wa Ligi Kuu ya Algeria ikiwa inawafuatia JS kabylie na imeshinda mara saba pia makombe mengine wakiwa wanashika nafasi ya tatu baada ya USM Alger na ES Setif.

Katika kipindi hiki, MCA ni kama timu ambayo imeamua kurejesha heshima yake.

Katika ligi wako katika nafasi ya nne, lakini wanaonekana wamepania kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.

Timu hiyo ina uwezo mkubwa na kamwe Yanga hawapaswi kwenda na hisia kuwa wao si USM Alger, Setif au Kabylie.

Bado wana nguvu, kwa wapinzani hao wakubwa wanaonekana ni vigogo na wana nguvu kubwa ya mashabiki ambao ni msukumo mkubwa wa wao kuendelea kufanya vizuri.


Yanga wanapaswa kuwa makini na kama maandalizi basi yawe bora. Lazima wajiandae hasa na lazima wawe jasiri kwa kutaka kufanya vema kwa kuwa hakuna kinachowezekana lakini haitakuwa rahisi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic