March 21, 2017


Baada ya Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe kuchukua namba ya kiungo kinda wa Madini FC, Awesu Awesu, dalili zinaonyesha hakuna ujanja, lazima atue Msimbazi.

Hans Poppe alichukua namba ya Awesu mara tu baada ya mechi dhidi ya Simba ambayo iliisha kwa Wekundu wa Msimbazi kushinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Laudit Mavugo.

Uamuzi wa Hans Poppe kuchukua nafasi ya Awesu inaonyesha kwamba mwanajeshi huyo mstaafu ni mtu asiye na maskhara na kama Awesu "hatazingu" basi ana nafasi ya kutua Msimbazi.

Simba ina viungo lukuki na mahiri lakini hadi kufikia Hans Poppe kuona hawezi kujivunga, maana yake njia yake ya kwenda Msimbazi ni nyeupeee.


Awesu alionyesha kiwango kizuri katika mechi hiyo na Hans Poppe kama kawaida yake, hakujivunga, akachukua namba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV