March 18, 2017





Waliokwenda kuiwakilisha Zanzibar pamoja na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) waliokuwa katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ulifanyika juzi Alhamisi nchini Ethiopia wamewasili nchini jana na kuweka bayana mambo yote yalijitokeza katika uchaguzi.

Moja kati ya mambo hayo ni pamoja na suala zima la Zanzibar kupata uanachama wa CAF nafasi ambayo ilikuwa kitafutwa kwa muda refu bila ya mafanikio. 

Lakini pia mbali na suala hilo viongozi walizungumzia kitendo cha Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kushindwa kufanya vizuri katika uchaguzi huo ambapo alikuwa akiwania nafasi ya Ujumbe wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).



Akizungumza na jana baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Rashid Ali Juma alisema kuwa wajumbe wote waliokuwa katika uchaguzi huo waliipigia kura Zanzibar kuwa mwanachama wa CAF.

Alisema baada ya Zanzibar kupewa uanachama alijikuta akitokwa na machozi  kwa kuona kitu alichokuwa akikihangaikiwa kimefanikiwa.

“Nawashukuru Watanzania wote. Kinachofuata sasa baada ya kupata uanachama wa Caf ulionifanya nitokwe na machozi baada ya kupata kura zote 54 za wajumbe wa mkutano huo, tunaingia katika harakati zingine za kuhakikisha tunapata uanachama wa Fifa ili siku moja Zanzibar nayo iweze kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa kama yalivyo mataifa mengine duniani,” alisema kiongozi huyo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic