March 30, 2017


Kikosi cha Simba sasa kina uhakika kutokana na ufiti wa kipa Manyika Peter.


Hali hiyo inaifanya Simba kuwa na uhakika hasa kwa kuwa hata kama kipa Daniel Agyei atakuwa na tatizo, bado Manyika atakuwa msaada mkubwa.


Kocha wa makipa wa Simba, Iddi Salim amesema Manyika yuko fiti na tayari kwa mechi yoyote.


“Unaona alivyo Agyei, badi ndivyo alivyo Manyika. Hii ni nzuri kwa timu yetu hata mmoja akiwa mgonjwa basi kuna uhakika wa asilimia mia mwingine kucheza na kufanya vizuri bila hofu.


“Lakini hata kipa mwingine huyu Denis, naye yuko vizuri kabisa. Lengo la hili ni kujihakikishia kwa asilimia mia katika upande wa kipa,” alisema Salim.


Hata hivyo, Manyika amekuwa hachezi kutokana na Agyei kuwa fiti zaidi na kuonyesha kiwango kizuri katika mechi nyingi.


Simba imebakiza mechi sita za Ligi Kuu Bara na kama itashinda zote, basi itajihakikishia ubingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV