March 28, 2017


Mashabiki wa Simba mkoani Kagera wamewashangaza wachezaji na viongozi walioambatana na msafara wa kikosi cha Simba mkoani humo.

Waliokuwa kwenye msafara huo wameshangazwa na shangwe na mapokezi makubwa waliyopewa.

Mapokezi hayo yanaashiria kweli mashabiki na wanachama wa Simba mkoani Kagera hasa wale walio Bukoba mjini, wanataka ubingwa.

Maana mashabiki hao walijitokeza kwa wingi, zaidi ya kilomita 20 kabla ya timu hiyo kuingia Bukoba mjini. Wakaipa mapokezi makubwa kwa misafara ya pikipiki na magari.

Simba imewasili mjini humo kujiandaa na mechi yao ya Aprili 2 dhidi ya Kagera Sugar.

Baada ya hapo, Simba itasafiri kwenda Mwanza kuivaa Mbao FC na baadaye Toto African.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV